ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE

ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE
CHUO BORA CHA UANDISHI WA HABARI TANZANIA

Wednesday, March 16, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA


 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wakimbizi wa Burundi walioko katika kambi ya  Lumasi  iliyopo wilayni Ngara. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15 2016.
 Baadhi ya wakimbizi wa Burundi walioko kwenye kambi ya Lumasi iliyopo wilayani Ngara wakimsikilza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2916.
 Waziri Mkuu, Kassim  Majliwa akiagana na viongozi kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Lumasi iliyoko Ngara  viongozi wa wilaya na UNHCR baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na waumishi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO baada ya kuwasili kwenye eneo unapowekwa mtambo mpya wa kufua umeme mjini Ngara ambao aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani.
 Moja ya mabango ambayo yalibebwa na wananchi wa Ngara katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Ngara Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wananchi wa Ngara baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Mtambo Mpya wa Umeme mjini Ngara Machi 15, 2016.
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Watumishi na Viongozi wa Mkoa wa Kagera kuhitimisha ziara yake mkoani humo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilay ya Ngara Machi 15, 2916. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

Nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa .

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu matokeo ya uripuaji wa mabomu na kuchoma moto nyumba na maskani za CCM Unguja na Pemba. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.Na Mwashungi Tahir na miza Kona - Maelezo Zanzibar      15/03/2016Nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa  na kitu kinachosadikiwa kuwa  ni bomu na watu wasiojulikana  majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani,...