ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE

ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE
CHUO BORA CHA UANDISHI WA HABARI TANZANIA

Thursday, April 21, 2016


Thursday, April 21, 2016

Wasomi wazungumzia staili ya Magufuli uteuzi wa Ma-DC

BAADA ya Rais John Magufuli, kuja na mtindo wa kuteua wakuu wa wilaya mmoja mmoja kujaza nafasi zilizo wazi badala ya kufanya mabadiliko kwa nchi nzima, baadhi ya wasomi wamepongeza hatua hiyo wakisema inasaidia kubana bajeti na kupata watu makini.
RAIS JOHN MAGUFULI.
Hivi Karibuni, Rais Magufuli alimteua, Gelasius Byakanwa, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kabla ya juzi kumteua Ally Hapi, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Humphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma.
Hatua hiyo ni tofauti na ya Marais waliotangulia ambao mara baada ya kuapishwa, walikuwa wakiteua Baraza la Mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi, wakuu wa mikoa wa wilaya nchi nzima.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kidiplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia, Israel Sostenes, alisema alichokifanya Rais Magufuli ni kujaza nafasi muhimu kwa upande wa watendaji na watawala.
“Ameshateua Baraza la Mawaziri, wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa idara nyeti, hatua mbayo ni nzuri, wakuu wa wilaya siyo jambo la muhimu sana kwa sababu ameshapanga vyema safu yake ya ngazi ya juu,” alisema.
Alisema Rais Magufuli ana nia njema na ya dhati na kwamba anaangalia na kufuatilia kwa makini kabla ya kuteua ili kupata wanaotosha kwenye nafasi hizo.
Alisema kuchelewa kwa uteuzi huo, hakuwezi kutokana na kukosekana kwa fedha bali ni kuona namna anaweza kuokoa fedha kwa kuteua wakuu wa wilaya.


Kwa upande wake, mchambuzi wa masuala ya siasa, Abdulhakim Atiki, alisema suala la kuteua wakuu kwa kujaza nafasi linatokana na Rais kuridhika na utendaji wa waliopo.
Alisema Baraza la Mawaziri ndiyo muhimu kwa sababu linavunjika, lakini kwa upande wa wakuu wa mikoa na wilaya wanaweza kuendelea kufanya kazi bila kuteua wapya.
“Huenda Rais ameona utendaji wao uko vizuri na akaishia kubadili wakuu wa mikoa pekee na wakuu wa wilaya akaendela kujaza nafasi. Hili ni jambo jema kwa sababu yuko makini na uteuzi wake,” alisema.
Naye Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda, alisema utaratibu huo alioufanya Rais Magufuli, ni jambo zuri kwani kitu cha msingi anachokiangalia ni utendaji wa kazi.
Alisema marais wanapoingia madarakani, wanakuwa na nafasi za uteuzi zaidi ya 5,000, hivyo Rais Magufuli anachokiangalia ni maslahi ya taifa na si vingine.
“Rais hajaingia kwa shinikizo la mtu ama kumchagua mtu kwa vile analipa fadhila, wapo wakuu wa wilaya ambao ni wazuri na amewabakiza hakuna umuhimu wa kuwaondoa wote, utaratibu mzuri ni kuangalia utendaji kazi kama ilivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alivyoachwa kulikuwa na sababu,” alisema Mbunda na kuongeza:
“Huu ni utaratibu mzuri wa utendaji kazi kwani anawafuatilia na baadaye kufanya uamuzi. Hii itasaidia kuongeza ufanisi wa kazi kwa viongozi wetu

Wednesday, March 16, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA


 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wakimbizi wa Burundi walioko katika kambi ya  Lumasi  iliyopo wilayni Ngara. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15 2016.
 Baadhi ya wakimbizi wa Burundi walioko kwenye kambi ya Lumasi iliyopo wilayani Ngara wakimsikilza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2916.
 Waziri Mkuu, Kassim  Majliwa akiagana na viongozi kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Lumasi iliyoko Ngara  viongozi wa wilaya na UNHCR baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na waumishi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO baada ya kuwasili kwenye eneo unapowekwa mtambo mpya wa kufua umeme mjini Ngara ambao aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani.
 Moja ya mabango ambayo yalibebwa na wananchi wa Ngara katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Ngara Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wananchi wa Ngara baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Mtambo Mpya wa Umeme mjini Ngara Machi 15, 2016.
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Watumishi na Viongozi wa Mkoa wa Kagera kuhitimisha ziara yake mkoani humo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilay ya Ngara Machi 15, 2916. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

Nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa .

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu matokeo ya uripuaji wa mabomu na kuchoma moto nyumba na maskani za CCM Unguja na Pemba. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.Na Mwashungi Tahir na miza Kona - Maelezo Zanzibar      15/03/2016Nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa  na kitu kinachosadikiwa kuwa  ni bomu na watu wasiojulikana  majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani,...

Saturday, January 30, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA MBIO ZA HAPA KAZI TU DODOMA HALF MARATHON

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mbio za Wabunge za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon zilizoanzia Bungeni hadi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016. Kushoyo kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson. Mwansasu (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Washiriki wa mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon wakishiriki mbio hizo mjini Dodoma Januari 30, 2016.
Mmoja wa wapigapicha walioshiriki mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon alilazimika kuomba msaada kwa askari wa usalama barabarani Mjini Dodoma Januari 30, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza wa mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon upande wa wanaume, Emmanuel Giriki kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya Pikipiki mshindi wa kwanza upande wa wanawake wa Mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon, Angela Davile (kulia) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma ambao wamedhamini pambano la mpira wa miguu kati ya wabunge na benki hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri Januari 30,2016. Benki hiyo pia ilitoa vifaa vya michezo kwa timu ya Bunge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa kikao cha haraka na viongozi wa vyama vya michezo nchini ili wamueleze kila mmoja amejipanga vipi kuinua viwango vya michezo katika chama chake.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Januari 30, 2016) wakati akizungumza na mamia ya viongozi na wakazi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma ambao walishiriki mashindano ya mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5) zilizofanyika leo mjini Dodoma.

Mashindano hayo yalijulikana kama “HAPA KAZI TU HALF MARATHON” yamefanyika ikiwa ni sehemu ya kuhimiza uchapakazi miongoni mwa Watanzania lakini pia ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kuadhimisha siku 100 za utendaji kazi tangu Rais John Pombe Magufuli alipoapishwa na kuanza kazi.

“Kuna maboresho yanaendelea ndani ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lakini haya yote hayawezi kufanikiwa kama viongozi wa michezo hawajajipanga vizuri. Ninatakata niandaliwe kikao cha siku moja na viongozi wa vyama vya michezo nchini ili waje wanieleze kila mmoja amejipanga vipi kuinua hali ya mchezo wake,” alisema huku akishangiliwa.

Alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania kwa kuandaa mbio hizo muhimu za kuhimiza Watanzania kuchapa kazi, lakini pia ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki katika mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika baadaye mwaka huu huko Rio de Janeiro, Brazil.

“Tunataka tuondokane na kauli ya Tanzania kuwa ni kichwa cha mwendawazimu na nipende kusisitiza kuwa maandalizi haya yasiwe ya mwisho bali yawe ya muda mrefu kwa sababu tunaenda kushiriki mashindano ya dunia. Nasema tena, tuache utamaduni wa maandalizi ya kukurupuka,” alisisitiza.

Aliwataka wadau mbalimbali wajitokeze kusaidia taasisi za michezo.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alishiriki mbio za km. 2.5 kuanzia saa 1 asubuhi, alikimbia kutoka eneo la Bunge hadi uwanja wa Jamhuri na kuzindua mashindano ya km. 21 saa 1:47 asubuhi na yale ya km. tano aliyazindua saa 1:51 asubuhi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alikabidhi pikipiki aina ya GSM kwa washindi wa kwanza wa nusu marathon, mabati 100 kwa washindi wa pili na mabati 40 kwa washindi wa tatu. Mshindi wa tatu hadi wa 10 kwa wanawake na wanaume walikabidhiwa fedha taslimu.

Washindi wa kwanza hadi wa tatu waliokabidhiwa zawadi na Waziri Mkuu upande wa wanawake ni  Anjelina Daniel (Pikipiki); Fadhila Salum (mabati 100) na Catherine Lange (mabati 40). Wote wanatoka mkoa wa Arusha.

Kwa wanaume walioshinda nafasi kama hizo ni Emmanuel Giniki (Katesh, Babati) aliyeshinda pikipiki; Gabriel Gerald wa Arusha (mabati 100) na Fabian Joseph wa Arusha (mabati 40).

Wakati huo huo, Benki ya CRDB Dodoma ilitoa zawadi za sh. 250,000/- kila mmoja kwa washiriki watatu ambao ni walemavu walioamua kushiriki mbio hizo mwanzo hadi mwisho. Waliokabidhiwa zawadi hizo na Waziri Mkuu ni Bw. Hassan Hussein Sharif, Bw, Christian Ally Amour na Bw. Shukuru Khalfani.

Benki hiyo ilikabidhi pia vifaa vya michezo kwa ajili ya timu ya wabunge kwa ajili ya pambano la soka linalotarajiwa kufanyika leo saa 10 jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma baina ya timu ya Bunge na timu ya CRDB. 

Dkt. Kigwangalla awapa funzo watumishi wa sekta ya afya, awataka kuwa wabunifu


Licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha sekta ya afya nchini, watumishi wa sekta ya afya wametakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu.
IMG-20160130-WA0029
Licha ya kutembelea wodi mbalimbali za wagonjwa, Dkt. Kigwangwala alitembelea maabara ya hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali, kushoto ni mtaalamu wa viwango vya maabara, Felix Zelote akimpatia maelezo waziri huyo
IMG-20160130-WA0030
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akitembelea Hospitali ya Mount Meru iliyopo mkoani Arusha.
Amesema hospitali zinatakiwa kusimama zenyewe kwa ukusanyaji wa mapato,hivyo upo ulazima wa kujenga au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo zitakua zenye ubora ambao unaweza kuwashawishi watu wenye pesa kuja kupata huduma kwenye hospitali za umma kuliko hivi sasa wanakimbilia hospitali binafsi.
"Hii itaifanya serikali kupata pesa ambazo sehemu kubwa zitatumika kuwahudumia watu wenye kipato cha chini hospitalini hapa,” alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema wateja wengi wanapokuja kupata huduma kwenye vituo vya huduma ya serikali,wanakata tamaa kwakuwa wanakuta hakuna watoa huduma, dawa wala vifaa tiba hivyo wanakimbilia huko kwenye hospitali binafsi.
"Lengo letu sio kuua hospitali binafsi bali tunataka muimarishe huduma za kulipia ili tupate pesa za kuwahudumia wasio na uwezo na ninyi watoa huduma wa serikali mpate sehemu yenu ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi,” alisema Dkt. Kingwangalla.
IMG-20160130-WA0032
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji
IMG-20160130-WA0027
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangwala akiwa amembeba mtoto mchanga (bado hajapatiwa huduma) na mama wa mtoto huyo Bi. Jamila Petro alipotembelea wodi ya wazazi hospitalini hapo
IMG-20160130-WA0028
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimuangalia mtoto huyo

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ, BALOZI WA TANZANIA KUWAIT NA KATIBU TAWALA WA KATAVI NA MWANZA LEO IKULU DAR ES SALAAM


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Dkt. 
Mahadhi Juma Maalim baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory  Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo baada ya kumuapisha  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve bvaada ya kumuapisha  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea saluti toka kwa Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kabla ya  kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi nyezo za kazi Kamishna wa Polisi  Paul Amani Moses Chagonja baada ya kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ MStaafu Luteni Jenerali (Rtd) Samuel Albert Ndomba baada ya shughuli ya kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifurhia jambo  na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ MStaafu Luteni Jenerali (Rtd) Samuel Albert Ndomba baada ya shughuli ya kiapo Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa JWTZ, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpongeza  Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja baada ya  kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpongeza Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo baada ya kumuapisha  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpongeza  Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve baada ya kumuapisha  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpongeza  Dkt. Mahadhi Juma Maalim baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya
 Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipena mikono na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  baada ya kuwaapisha Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipena mikono na Inspekta Jenerali wa Polisi Afande Ernest Mangu baada ya kuwaapisha Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ mpya  Luteni Jenerali Venance Salvatory  Mabeyo  na  Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Mstaafu Luteni Jenerai (rtd) Samwel Ndomba Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Mnadhimu Mkuu wa JWTZ mpya  Luteni Jenerali Venance Salvatory  Mabeyo  na  Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Mstaafu Luteni Jenerai (rtd) Samwel Ndomba Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  akifurahia jambo na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi  baada ya kuwaapisha  Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufulia akiongea na viongozi  baada ya kuwaapisha Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na   Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja baada ya  kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na msemaji wa JWTZ Luteni Kanali Ngeleba  Lubinga baada ya kuwaapisha Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahman Kaniki baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na  Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016