ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE

ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE
CHUO BORA CHA UANDISHI WA HABARI TANZANIA

Saturday, January 30, 2016

Dkt. Kigwangalla awapa funzo watumishi wa sekta ya afya, awataka kuwa wabunifu


Licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha sekta ya afya nchini, watumishi wa sekta ya afya wametakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu.
IMG-20160130-WA0029
Licha ya kutembelea wodi mbalimbali za wagonjwa, Dkt. Kigwangwala alitembelea maabara ya hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali, kushoto ni mtaalamu wa viwango vya maabara, Felix Zelote akimpatia maelezo waziri huyo
IMG-20160130-WA0030
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akitembelea Hospitali ya Mount Meru iliyopo mkoani Arusha.
Amesema hospitali zinatakiwa kusimama zenyewe kwa ukusanyaji wa mapato,hivyo upo ulazima wa kujenga au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo zitakua zenye ubora ambao unaweza kuwashawishi watu wenye pesa kuja kupata huduma kwenye hospitali za umma kuliko hivi sasa wanakimbilia hospitali binafsi.
"Hii itaifanya serikali kupata pesa ambazo sehemu kubwa zitatumika kuwahudumia watu wenye kipato cha chini hospitalini hapa,” alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo alisema wateja wengi wanapokuja kupata huduma kwenye vituo vya huduma ya serikali,wanakata tamaa kwakuwa wanakuta hakuna watoa huduma, dawa wala vifaa tiba hivyo wanakimbilia huko kwenye hospitali binafsi.
"Lengo letu sio kuua hospitali binafsi bali tunataka muimarishe huduma za kulipia ili tupate pesa za kuwahudumia wasio na uwezo na ninyi watoa huduma wa serikali mpate sehemu yenu ili muweze kufanya kazi kwa ufanisi,” alisema Dkt. Kingwangalla.
IMG-20160130-WA0032
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji
IMG-20160130-WA0027
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangwala akiwa amembeba mtoto mchanga (bado hajapatiwa huduma) na mama wa mtoto huyo Bi. Jamila Petro alipotembelea wodi ya wazazi hospitalini hapo
IMG-20160130-WA0028
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimuangalia mtoto huyo

No comments:

Post a Comment