SERIKALI
yaombwa kuchangia chakula cha watoto wakiwa shule ili kuwasaidia kusoma
wakiwa wameshiba kwani watoto hawawezi kusoma wakiwa na matumbo hayana
chakula.
Hayo yamesemwa na Shule
kuu ya Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Joviter Katabaro wakati
akichangia maada katika mkutano wa kujadili masuala ya elimu katika
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyrere jijini Dar es Salaam
leo.
Nae
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Haki Elimu, John Kalage kuwa
wamependekeza Lugha ya Kiswahili na Kiingereza iwe lugha ya kufundishia
na kujifunzia kwa ngazi zote ili kuboresha mazingira ya kufundishia na
kujifunzia.
Pia ametoa wito kwa serikali kuwa kutoa elimumsingi bure sabamba na kupunguza michango ya wazazi mashuleni.
Aidha
Karage amesema kuwa ili kuhakikisha ubora mashuleni, shule, taasisi na
vyuo vinapaswa kufanyiwa ukaguzi kuhusu ufundishaji na ujifunzania
pamoja na mazingira kuwa mazuri.
Mhadhiri
wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bashiru Ally akizungumza na
wadau wa elimu leo jijini Dar es Salaam wakati wakijadiliana kuhusiana
na masuala mbalimbali ya elimu kwa watoto waliotolewa fedha na Serikali
kwaajili ya kutolewa elimu bure kwa elimu ya Sekondari na Shule za
msingi. Kulia ni Profesa Mshiriki wa chuo kikuu cha Dodoma, Profesa
Willy Komba.
Profesa
Mshiriki wa chuo kikuu cha Dodoma, Profesa Willy Komba akizungumza na
wadau wa Haki elimu leo wakati wa kijadili Lugha gani itumike katika
kufundishia kwa wanafunzi wa shule za hapa nchini.ilikwa alisema sema
kuwa wanafunzi wasichanganyikiwe kuhusiana na lugha ambayo itatumika
kufundishia kwa masomo yao.
Meneja
wa Idara ya Utafiti na uchambuzi wa Haki Elimu akizungumza na wadau wa
elimu leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Kulia ni Shule kuu ya Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Joviter
Katabaro akiwa katika mkutano huo wa wadau wa elimu.
Profesa
Mshiriki Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Martha Qorro akizungumza
katika uzinduzi wa ripoti ya haki elimu iliyozinduliwa leo katika ukumi
wa mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam kuhusiana na namna gani
serikali itoe uchangauzi wa pesa zilizotolewa kwa shule za msingi na
sekondari zitumikwa kwa namna ani na mawanyo wake upoje ili kila
mwananchi ajue hizo pesa zimetolewa kwa matumizi gani.
Baadhi ya wadau wa elimu wakiwa katika mkutano huo wa kujadili masuala ya elimu uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii
No comments:
Post a Comment